Home Sports KOCHA MPYA SIMBA QUEENS ATAJA KILICHOMLETA BONGO

KOCHA MPYA SIMBA QUEENS ATAJA KILICHOMLETA BONGO

KOCHA mpya wa Simba Queens, Charles Ayiekoh Mbuzi ameweka wazi sababu ya kujiunga na timu hiyo.

Kocha huyo ameeleza jinsi viongozi wa Simba walivyoanza mchakato wa yeye kujiunga na Simba Queens hadi akamwaga wino.

“Mara baada ya mchezo wa fainali dhidi ya Simba Queens, uongozi wa Simba ulipendezwa na uwezo wangu ambapo meneja Selemani Makanya alinipa mwaliko kukutana kuweza kuongea.”

“Nilivutiwa na jinsi walivyoheshimu uwezo wangu na kukubali mahitaji yangu ambayo niliyapendekeza, tulikubaliana kuwa kama yatatimizwa nitajiunga nao, ikawa hivyo na ndio maana nipo hapa,”.

Ayiekoh ni kocha mwenye wasifu bora nchini Uganda amewahi kufundisha timu kubwa kama URA,Vipers na kwenye soka la wanawake ni msimu wake wa kwanza na amebeba ubingwa wa ligi ya ndani na She Corporate huku akifanikiwa kufika fainali ya CECAFA ambapo walifungwa na Simba Queens.

Previous articleIHEFU YAAMBULIA POINTI LIGI KUU BARA
Next articleYANGA YAMTEKA BOSI WA AL HILAL, SIMBA KUWAFUATA WAANGOLA KITEMI