Home Sports SHABIKI WA SIMBA ASHINDA MILIONI 49 NA10 BET

SHABIKI WA SIMBA ASHINDA MILIONI 49 NA10 BET

SHABIKI wa Klabu ya Simba na timu ya Manchester United, Derick Mustafa, ameshinda Sh 49.8 milioni baada ya kubashiriki kwa kwa usahihi mechi 14 za ligi mbalimbali za soka duniani kupitia ‘mkeka’ wa kampuni ya 10 Bet.

Mustafa ambaye ni mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kushinda kiasi kikubwa cha fedha kutokana na kupata ugumu katika baadhi ya mechi zilizokuwa zinachezwa.

Amesema mechi iliyompa wakati mgumu zaidi ni kati ya Manchester United na Sheriff Tiraspol zilizokuwa zinacheza mchezo wa ligi ya Europa na Manchester United kuibuka washindi wa mabao 2-0 kwenye uwanja wa ugenini.

Kwa mujibu wa Mustafa, timu hizo zilikuwa na uwiano sawa na alikuwa na wasiwasi wa timu yake kutokana na matokeo ya nyuma ambayo hayakuwa mazuri.

“Nilitumia uzoefu wangu katika kutabiri mechi hiyo na baadaye kupatia ambapo Manchester United ilishinda mabao 2-0. Nilifurahi kwani mbali ya ushindi nimeweza kupata fedha kwa kupitia 10Bet,” amesema Mustafa.

Alieleza kuwa fedha hizo atazitumia kuboresha biashara yake ndogo kwa kuongeza kwenye mtaji na kupanua mtandao wake wa masoko.

“Nitatumia fedha hizi kuanzisha na kuboresha miradi yangu mbalimbali ya ujasiriamali. Ni faraja kwangu kushinda kiasi hiki kikubwa cha fedha. Lazima nichanganue aina ya biashara ninayoenda kufanya, faida na changamoto zake kabla ya kuamua chochote,” amesema.

Meneja masoko wa 10Bet Tanzania George Abdulrahman amesema Mustafa anakuwa mshindi wa kwanza kujishindia mamilioni ya pesa kupitia kampuni yao.

Abdulrahman amesema 10 BET ina bonasi kubwa zaidi barani Afrika yenye asilimia 1,000 ambayo inamwezesha mtu anayebashiri kushinda fedha nyingi zaidi kwenye ushindi wake.

“Mustafa alifanikiwa kuweka dau lake lililomwezesha kushinda Sh49.8m kupitia ‘bonus yetu ya ‘multibet’ ya asilimia elfu moja, tunatoa rai kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 kubashiri na 10bet ili kuweza kushindia fedha nyingi katika kupitia mkeka mmoja na zaidi. Unachotakiwa kufanya ni kutembelea www.10bet.co.tz, au kupitia app yetu na USSD *149*00#,  ” amesema Abdulrahman.

Previous articleVIDEO: MWARABU ALIYEPIGWA NA KIDUKU AANZA VISINGIZIO
Next articleBURUDANI SAWA, MANDONGA UTANI WAKE USIVUKE MIPAKA