Home International HAALAND AWEKA REKODI PREMIER

HAALAND AWEKA REKODI PREMIER

ERLING Haaland mshambuliaji wa Manchester City wakati timu yake ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Wolves ugenini ameandika rekodi nyingine tena.

Ni bao la Jack Grealish dakika ya kwanza kisha likapachikwa bao na Haaland mwenyewe dakika ya 16 na lile la tatu ilikuwa ni kazi ya Phil Foden dakika ya 69.

Nyota huyo anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza ndani ya Ligi Kuu England kufunga mechi nne za mwanzo ugenini.

Pia kwa mara ya kwanza staa huyo alifanikiwa kufunga bao nje ya boksi na mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa ni Agosti 14,2021 akiitumikia Borussia Dortmund kwenye mchezo dhidi ya Eintracht Frankfurt.

Kwenye michuano yote nyota huyo ametupia mabao 14 na sasa Arsenal imeshushwa kileleni na City ikiwa na pointi 17 huku Wolves wao wakikamilisha dakika 90 pungufu baada ya beki wao Nathan Collins kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 33 kwa kumchezea faulo Grealish.

Previous articleKOCHA SIMBA ANA HISTORIA YA JWANENG GALAXY WALICHOWAFANYA
Next articleSAUTI:PHIRI AFUNGUKIA BAO LAKE CAF