Home Sports KOCHA SIMBA ANA HISTORIA YA JWANENG GALAXY WALICHOWAFANYA

KOCHA SIMBA ANA HISTORIA YA JWANENG GALAXY WALICHOWAFANYA

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema vijana wake wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Big Bullets.

Mgunda amebainisha kuwa historia yakufungwa nyumbani msimu uliopita wa 2021/22 na kutolewa katika hatua za awali anazo hata wachezaji wanajua kuhusu hilo.

Huu ni mchezo wa marudio wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali baada ya ule wa kwanza uliochezwa Malawi, Simba kushinda mabao 2-0.

Mgunda ameweka wazi kuwa alisimuliwa historia ya Simba kupoteza mchezo wa kimataifa ikiwa nyumbani dhidi ya Jwaneng Galaxy baada ya kutoka kushinda ugenini.

“Maandalizi yamekamilika Mungu awajalie vijana waamke salama ili washinde mchezo wetu ambao ni muhimu.

“Historia nimeipata kuna makosa yalifanyika huko nyuma kwa sasa tumeyafanyia kazi ili yasijirudie.

“Tupo tayari kwa mchezo kwenye kila idara tumefanyia kazi makosa yetu ikiwa ni pamoja na upande wa uimara kwenye mapigo huru pamoja na ulinzi, mashabiki wajitokeze kwa wingi,” amesema.

Nyassa Big Bullets nao wanahitaji ushindi kwenye mchezo wa leo unaitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Previous articleUKUTA WA WANANCHI MGUMU DAKIKA 180 KIMATAIFA
Next articleHAALAND AWEKA REKODI PREMIER