Home Sports UKUTA WA WANANCHI MGUMU DAKIKA 180 KIMATAIFA

UKUTA WA WANANCHI MGUMU DAKIKA 180 KIMATAIFA

UKUTA wa Yanga kimataifa ndani ya dakika 180 haujaokota bao katika hatua za awali mbele ya Zalan FC.

Mchezo wa kwanza nyota wa Yanga ikiwa ni pamoja na Dickosn Job, Bakari Mwamnyeto, Kibwana Shomari hawakuokota bao sawa na ule wa pili, yote ilichezwa Uwanja wa Mkapa.

Ni mabao 9 wameweza kufunga Yanga na kinara wao ni Fiston Mayele ambaye katupia mabao 6, kwenye kila mchezo alitupia hat trick.

Ushindi huo unaifanya Yanga kusonga mbele hatua inayofuata na wanatarajiwa kukutana na mshindi wa mchezo kati ya St George ama Al Hilal hatua inayofuata.

Wakipenya hapo safari inaelekea katika hatua ya makundi ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ushirikiano na kufuata maelekezo ni mambo yanayowapa matokeo.

“Kila mchezaji anajua kazi yake na wanashirikiana, kikubwa ni kuona tunapata matokeo kwenye mechi ambazo tunacheza,”.

Mchezo wa pili jana Septemba 17, Yanga ilishinda mabao 5-0 ambapo Mayele alifunga matatu, Farid Mussa na Aziz KI hawa walitupia mojamoja.

Previous articleYANGA HAISHIKIKI, MAYELE AWEKA REKODI CAF,PHIRI HAPOI
Next articleKOCHA SIMBA ANA HISTORIA YA JWANENG GALAXY WALICHOWAFANYA