Home International NAPOLI WAICHAPA LIVERPOOL 4G

NAPOLI WAICHAPA LIVERPOOL 4G

USIKU wa Ligi ya Mabingwa Ulaya umewapa furaha Napoli wakiwa Uwanja wa Diego Armando Maradona kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Liverpool.

 Ni mchezo wa kwanza kwa  Kundi A ambapo Liverpool hawajaamini ambacho wamekiona licha ya kupewa nafasi kubwa ya kuweza kupata ushindi kwenye mchezo huo.

Mabao ya Napoli inayoongoza kundi ikiwa na pointi tatu ni mali ya Piotr Zielinok aliyepachika kimiani mabao mawili ilikuwa dakika 5, (p), 47, Andre-Frank Zambo Anguissa dakika ya 31 na Giovanni Simeone dakika ya 44.

 Kwa Liverpool ni bao la Luis Diaz dakika ya 49 lilikuwa lakufutia machozi katika mchezo huo.

Mashuti ya Napoli ambayo waliweza kupiga ilikuwa ni 18 na yalilenga lango mashuti 7 na Liverpool 15 na yalilenga lango mashuti 7.

Previous articleSAUTI: SIMBA YATANGA KOCHA MPYA USIKU,KUANZA KAZI KIMATAIFA
Next articleMABOSI SIMBA WAVUTANA KISA KOCHA MPYA,MKATABA WAMBANA BM