JKT Tanzania vs Yanga SC ni kivumbi

JKT Tanzania vs Yanga SC ni kivumbi Mei 16, 2026 Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo kwa wababe hawa wawili kusaka tiketi kutinga hatua ya nusu fainali.

Mabingwa watetezi ni Yanga SC kwenye taji hili hivyo wataingia uwanjani wakiwa na hesabu za kutetea taji hilo huku JKT Tanzania wakiwa na hesabu kutinga hatua ya nusu fainali.

Rekodi zinaonyesha kuwa 2025 wakati Yanga SC inatinga hatua ya fainali iliwafunga JKT Tanzania hatua ya nusu fainali hivyo mchezo wa kesho ni kisasi na mwendelezo wa rekodi.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.