2JNRW2R 13 Aug 2022 - Brentford v Manchester United - Premier League - Gtech Community Stadium
Manchester United Manager Erik ten Hag during the Premier League match at the Gtech Community Stadium, London.
Picture : Mark Pain / Alamy Live News
INAELEZWA kuwa Kocha Mkuu wa Manchester United, Eric ten Hag anafikiria kumpiga benchi nahodha wa timu hiyo, Harry Maguire.
Itakuwa ni kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Old Trafford.
Mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa unatarajiwa kuchezwa Jumatatu ijayo.
Nyota huyo ameanza kwenye mechi mbili ambazo timu hiyo imecheza lakini wameambulia maumivu kwa kichapo mbele ya Brighton na Brentford na kwa sasa ipo mkiani.
Inaelezwa kuwa kocha huyo anafikiria kumuanzisha Martinez pamoja na Raphael Varane.