Home International SOPU APEWA TUZO, KUIKOSA KAGERA SUGAR LEO

SOPU APEWA TUZO, KUIKOSA KAGERA SUGAR LEO

KIUNGO Abdul Suleiman ambaye ni ingizo jipya ndani ya Azam FC, alipewa zawadi ya kuku na shabiki wa Azam FC hivi karibuni, leo Agosti 17 atakosekana kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar kwa kuwa alipata maumivu kwenye mazoezi.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa mchezaji huyo alipata maumivu baada ya timu kurejea kambini Misri ilipokuwa kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2022/23.

Sopu aliibuka ndani ya Azam FC akitokea kikosi cha Coastal Union ambapo alikuwa ni mchezaji bora kwenye Kombe la Shirikisho na mfungaji bora na alikuwa kwenye kikosi bora cha ligi msimu wa 2021/22.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa ligi dhidi ya Kagera Sugar na tunajua kwamba utakuwa ni mgumu na wenye ushindani mkubwa ila tupo tayari kwani maandalizi yapo vizuri.

“Atakosekana Sopu alipata maumivu kwenye mazoezi baada ya kurejea Misri ila anaendelea vizuri kwa sasa pia Idd Suleiman, huyu alikuwa akipata matibabu kwa muda tayari yupo fiti ila mchezo wa Kagera Sugar ataukosa mpaka mechi zijazo,” amesema Thabit.

Previous articleKELVIN NASHON:TUTATUMIA PLAN B KUIKABILI SIMBA
Next articleKIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA DHIDI YA GEITA GOLD UWANJA WA MKAPA