Home Sports KELVIN NASHON:TUTATUMIA PLAN B KUIKABILI SIMBA

KELVIN NASHON:TUTATUMIA PLAN B KUIKABILI SIMBA

 KIUNGO wa Geita Gold, Kelvin Nashon amesema kuwa anatambua wapinzani wao Simba ni imara lakini wao wataingia na plan mbili ikifeli ya kwanza watatumia ya pili ili kupata matokeo.

Leo Agosti 17,2022 Simba inatarajiwa kuwakaribisha Geita Gold kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.

Unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu zote mbili ndani ya ligi kwa msimu huu wa 2022/23.

Kiungo huyo mzawa amesema:- “Tunacheza na Simba tunatambua kwamba ni timu imara na kubwa lakini tumejipanga kuweza kukabiliana nao, tuna plan A na B ikifeli A tutatumia B.

“Ambacho tunahitaji ni kupata ushindi kwani ligi itakuwa na ushindani mkubwa, tunakumbuka kwamba msimu uliopita tulishindwa kupata pointi tatu mbele ya Simba huu ni msimu mwingine.

“Kitakachotokea ni sehemu ya mchezo na kila mmoja anatambua tunahitaji ushindi kuanzia wachezaji wote morali ni kubwa na tutajitahidi kucheza kwa heshima kuikabili Simba kwani licha ya kwamba ametoka kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii bado anabaki kuwa Simba,” amesema.

Previous articleMZUNGU WA SIMBA ABAINISHA ATAREJESHA FURAHA KWA MASHABIKI
Next articleSOPU APEWA TUZO, KUIKOSA KAGERA SUGAR LEO