Home Sports MZUNGU WA SIMBA ABAINISHA ATAREJESHA FURAHA KWA MASHABIKI

MZUNGU WA SIMBA ABAINISHA ATAREJESHA FURAHA KWA MASHABIKI

MZUNGU wa Simba,Dejan Georgejick amesema kuwa anaumia kuona kwamba timu hiyo imepoteza kwa kufungwa mbele ya Yanga hivyo anaahidi kwamba atarejesha furaha kwa kuwa anatambua kila kitu kinawezekana.

Mshambuliaji huyo amecheza mechi mbili ilikuwa moja ya kirafiki dhidi ya St George na moja ilikuwa ni ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga ambapo walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

Kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya St George,Simba ilishinda mabao 2-0 Uwanja wa Mkapa ilikuwa Agosti 8 kwenye kilele cha Simba Day.

Mserbia huyo amesema: “Licha ya kwamba nimekuwa kwenye familia ya Simba kwa muda mfupi ninapata maumivu kwa kuweza kupoteza kwenye mchezo wetu uliopita na ninajihesabu kwamba mimi nimezaliwa kwenye familia ya ushindi.

“Nimezaliwa kutoka kwenye nchi ya watu wenye asili ya kushinda kama ilivyo kwa mcheza tenisi wa Serbia ambaye ni Novak Djokovic hivyo kwa yale ambayo yametokea nimeona ni maumivu ila bado kuna nafasi ya kuweza kufanya vizuri.

“Kwa heshima ya watu milioni wa Simba ambao ni mashabiki nitapambana na nitajitoa kwa moyo kwa ajili ya kufanya kila linalowezekana ili kupata kile kilicho bora kwa ajili ya timu, kufunga mabao na kuwapa furaha wale ambao wapo pamoja na sisi ninafurahi kuwe kwenye upande wa kushinda daima,” .

Leo Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Zoran Maki ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Geita Gold kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Previous articleMSAKO WA POINTI TATU ZA YANGA MBELE YA POLISI TANZANIA
Next articleKELVIN NASHON:TUTATUMIA PLAN B KUIKABILI SIMBA