Home International ARSENAL WAANZA KWA KASI LIGI KUU ENGLAND

ARSENAL WAANZA KWA KASI LIGI KUU ENGLAND

 ARSENAL wameanza Ligi Kuu England kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Crystal Palace ugenini watupiaji walikuwa ni Gabriel Martinell dk ya 20 na Marc Guehi OG dk ya 85.

Arsenal inakuwa ni timu ya kwanza msimu wa 2022/23 kuweza kufunga na kuongoza ligi.

Mbali na hilo kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Selhurst Park nyota wa Arsenal alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.

 Jina lake ni William Saliba ambaye aliweza kuonesha ubora wake kwenye mchezo huo wa msimu mpya wakati Arsenal ikisepa na pointi tatu mazima ugenini.

Previous articlePOLISI TANZANIA INASHUSHA WAPYA KWA KASI
Next articleWIKI YA MWANANCHI NI LEO UWANJA WA MKAPA