Home Sports WIKI YA MWANANCHI NI LEO UWANJA WA MKAPA

WIKI YA MWANANCHI NI LEO UWANJA WA MKAPA

AGOSTI 6,2022 leo ni kilele cha Wiki ya Mwananchi ambayo ilikuwa imeambatana na matukio ya kurejesha kwa jamii.

Pitso Mosimane kocha mwenye uzoefu na mechi za kimataifa Afrika ambaye ni raia wa Afrika Kusini ni miongoni mwa watakaoshudia mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa Yanga inayonolewa na Nasreddine Nabi dhidi ya Vipers FC ya Uganda.

Mosimane ambaye alikuwa kocha wa Al Ahly kabla ya kuamua kubwaga manyanga yupo kwenye ardhi ya Tanzania baada ya kupewa mualiko na Yanga.

Siku ya leo Yanga inatarajia kuweza kufanya utambulisho wa wachezaji wake wapya na wale ambao walikuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu uliopita.

Mbali na wachezaji pia uzi mpya utatambulishwa leo kwa mashabiki baada ya kuweza kuzinduliwa mapema na mashabiki wengi wameanza kununua uzi huo.

Jana wachezaji wa Yanga ikiwa ni pamoja na Yanick bangala, MVP,Aziz KI ni miongoni mwa wachezaji ambao walifanya mazoezi ya mwisho ya maandalizi ya mchezo wao.

Previous articleARSENAL WAANZA KWA KASI LIGI KUU ENGLAND
Next articleMAKOCHA SIMBA NA YANGA KUIBIANA MBINU KWA MKAPA