Home Sports POLISI TANZANIA INASHUSHA WAPYA KWA KASI

POLISI TANZANIA INASHUSHA WAPYA KWA KASI

IKIWA kwenye maboresho ya kikosi chao kwa msimu wa 2022/23 Klabu ya Polisi Tanzania imemalizana na kiungo wa kimataifa Ambroes Awio raia wa Ugada pamoja na mzawa Khamis Kanduru.

Wote wawili  wamesaini  mkataba wa miaka miwili hivyo kwa msimu ujao watakuwa ndani ya kikosi hicho ambacho kimeweka kambi Dar.

Msimu uliopita Awio alikuwa ndani ya kikosi cha Biashara United ya Mara ambayo imeshuka daraja na msimu ujao itashiriki Championship.

Mbali na hao pia Polisi Tanzania imemtamulisha Fredy Tangalo ambaye alikuwa ndani ya Namungo FC msimu uliopita.

Mwingine mpya ndani ya kikosi hicho ni beki Hassan Kapona ambaye ni miongoni mwa wachezaji walioipandisha timu hiyo kutoka Ligi Daraja la Kwanza.

Ofisa Habari wa Polisi Tanzania,Hassan Juma amesema kuwa wanahitaji kuwa na kikosi imara na cha ushindani.

“Tunatambua kwamba ushindani utakuwa mkubwa nasi pia tunakuja kupambana ili kuweza kufanya vizuri kwenye mechi zetu ambazo tutacheza,”.

Previous articleLEO NI BYUTIBYUTI,SIMBA YAMSHUSHA MSERBIA
Next articleARSENAL WAANZA KWA KASI LIGI KUU ENGLAND