Home Sports MTUNISIA FRESH YANGA,KAZI INAANZA KESHO

MTUNISIA FRESH YANGA,KAZI INAANZA KESHO

MTUNISIA Nasreddine Mohammed Nabi ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo ya ‘Wananchi’ hadi mwaka 2024.

Licha ya Nabi kuhitaji ongezo zaidi la mshahara ambao wameafikiana, kingine ni mipango yake ndani ya mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania.

 Nabi anaamini anaweza kupata mafanikio aliyokosa alikopita, kama Yanga wanavyoamini pia juu yake hasa kufuatia kuimarishwa kwa kila idara ndani ya kikosi hicho msimu huu.

Nabi ameiongoza Yanga kutwaa mataji matatu muhimu msimu uliopita ambayo yalikwenda kwa watani zao wa jadi Simba.

Baada ya kusaini kandarasi hiyo, Nabi amesema; “Bado nipo nipo sana, safi fresh.

Msimu uliopita  Nabi aliongoza Yanga kutwaa Ngao ya Jamii ubingwa wa ligi kuu ambao walimaliza bila kufungwa, Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation).

Kesho anatarajia kukiongoza kikosi hicho kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Vipers FC ya Uganda.

Previous articleSHIGONGO ANOGESHA WIKI YA SIMBA DAY BUCHOSA
Next articlePABLO FRANCO AIBUKA KWA MTINDO HUU SIMBA