Home Sports SHIGONGO ANOGESHA WIKI YA SIMBA DAY BUCHOSA

SHIGONGO ANOGESHA WIKI YA SIMBA DAY BUCHOSA

WANACHAMA na mashabiki wa Simba SC, Buchosa nao ni miongoni mwa wale ambao wanaendelea na shughuli za kijamii kabla ya maadhimisho ya Simba Day,Agosti 8,Uwanja wa Mkapa

Wanachama hao ambao ni kutoka tawi la Simba Buchosa limeadhimisha sherehe hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii zilizohudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric Shigongo.

Akizungumzia na mashabiki wa Simba wa Jimbo hilo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Luchili, Shigongo amewapongeza viongozi, wanachama na mashabiki wote wa Simba Buchosa kwa kufanya jambo ambalo linaleta hamasa ya kukuza michezo na kuijali jamii.

“Kwa hili jambo ni kubwa hasa kwa kuijali jamii na kuendelea kuwa karibu na jamii hivyo linapaswa kuwa na mwendelezo kila wakati.Nina amini kwamba kwa namna ambavyo Simba imeweza kufanya usajili itakuwa na msimu mzuri kwenye mashindano yake kimataifa,” amesema.

Msimu uliopita wa 2021/22 Simba ilikamilisha ligi ikiwa nafasi ya pili na ile ya kwanza ilikuwa kwa watani zao wa jadi Yanga ambao walitwaa ubingwa wa ligi.

Previous articleST GEORGE SC MABINGWA WA ETHIOPIA KUCHEZA NA SIMBA
Next articleMTUNISIA FRESH YANGA,KAZI INAANZA KESHO