Home Sports ST GEORGE SC MABINGWA WA ETHIOPIA KUCHEZA NA SIMBA

ST GEORGE SC MABINGWA WA ETHIOPIA KUCHEZA NA SIMBA

MABINGWA wa Ligi Kuu ya Ethiopia, Saint George S.C watakuwa Dar kwenye mchezo wa Simba Day Agosti 8.

Siku hiyo itakuwa ni maalumu kwa ajili ya Klabu ya Simba kuweza kutamulisha wachezaji wapya pamoja na uzi mpya.

Pia itakuwa ni siku ya kutambulisha benchi jipya la ufundi ambapo kwa sasa Kocha Mkuu ni Zoran Maki ambaye alikuwa na kikosi nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2022/23.

Mwingine ambaye ni mpya ni kocha wa makipa ambaye ametambulishwa ndani ya Simba anaitwa Mohamed Rachid.

Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba,Ahmed Ally amesema kila kitu kinakwenda sawa na leo wanaendelea kurejesha kwa jamii.

“Tupo kwenye Wiki ya Simba na tunaendelea kurejesha kwa jamii,kila mmoja anatambua kwamba tunajambo letu hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema.

Previous articleBAADA YA OKWA,SIMBA IMEKAMILIKA,YANGA YAPIGA TIZI LA KUFA MTU
Next articleSHIGONGO ANOGESHA WIKI YA SIMBA DAY BUCHOSA