Home Sports KMC YASHUSHA PRESHA KWA MASHABIKI WAKE

KMC YASHUSHA PRESHA KWA MASHABIKI WAKE

UONGOZI wa KMC umewataka mashabiki wasiwe na presha juu ya usajili wao kwa kuwa wanajua kile ambacho wanafanya.

 Kwa sasa KMC inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery imekuwa ikiwapukutisha mastaa wake ambao mikataba yao imeisha na wengine kupata madili mapya kwa msimu ujao.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wanatambua kile ambacho wanakifanya wakati ukifika kila kitu kitakuwa hadharani.

“Kuna mchezaji tulimuacha anaitwa Hassan Kabunda nilipokea simu nyingi juu yake lakin sio huyo tumewaacha wachezaji wengi kuna sababu na wale ambao wataachwa tutawatangaza kisha tutaanza kusajili wengine.

“Hatuna fujo sisi tunafanya kwa umakini na hakuna haja ya kuwa na presha kila kitu kitakuwa sawa na tunaamini kwamba mambo yatakuwa bomba kabisa,” amesema.

Miongoni mwa nyota ambao wameachwa ni pamoja na Hassan Kessy,Nickson Kibabage na Hassan Kabunda.

Previous articleSIMBA WAIVUTIA KASI YANGA NGAO YA JAMII
Next articleAZAM KUKIWASHA LEO MISRI KWA MARA YA KWANZA