Home Sports SIMBA WAIVUTIA KASI YANGA NGAO YA JAMII

SIMBA WAIVUTIA KASI YANGA NGAO YA JAMII

MKUU wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba,Ahmed Ally ameweka wazi kuwa wanatafuta pumzi ya moto ambayo itashushwa Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wao wa Ngao ya Jamii.

Simba imeweka kambi Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2022/23 na wanatarajia kurejea Agosti 3 kwa ajili ya maandalizi ya Simba Day,Agosti 8.

 Ally amesema kuwa wanatambua msimu uliopita hawakujafanya vizuri hivyo ni muda wa kuandaa pumzi ya moto na wataanza na Ngao ya Jamii.

“Muda wetu sasa wa kuandaa pumzi ya moto na hiyo itakuwa ni kwa ajili ya msimu mzima ,ukiangalia hatukuwa na mwendo mzuri msimu uliopita sasa tunarudi na kazi itakuwa kwenye mchezo wetu wa Ngao ya Jamii.

“Benchi la ufundi linatambua kwamba mchezo wetu wa Ngao ya Jamii utakuwa dhidi ya watani zetu hivyo mwanzo wetu utatufanya tuweze kuwa kwenye ubora zaidi,tunawaheshimu wapinzani na tunajua ushindani utakuwa mkubwa,” amesema Ally.

Kikiwa nchini Misri kikosi cha Simba kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2022/23 wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Haras El Hodoud.

Previous articleMANARA ANAVYOGOMBANA NA MANARA MWENYEWE
Next articleKMC YASHUSHA PRESHA KWA MASHABIKI WAKE