Home International NEYMAR JR AGOMEA ISHU YA KUONDOKA PSG

NEYMAR JR AGOMEA ISHU YA KUONDOKA PSG

 NYOTA wa Klabu ya PSG,Neymar Jr amebainisha kuwa anataka kubaki ndani ya timu hiyo japo hakuna ambaye amezungumza naye kujua hatma yake.

Mkataba wake ndani ya PSG unatarajiwa kumeguka mwaka 2026 amekuwa akitajwa kwamba anaweza kuuzwa katika kikosi hicho.

Staa huyo alisajiliwa na PSG kwa rekodi kubwa ilikuwa ni 2017 akitokea Barcelona anatajwa kuwa anaweza kuuzwa hapo kuisuka PSG.

Tangu ametua hapo amekuwa akiwa ni mtu wa kuuguza majeraha mara kwa mara ndani ya timu hiyo.

“Nataka kubaki hapa PSG hakuna mtu yeyote ndani ya PSG ambaye ameniambia jambo lolote kuhusu hatma yangu ila mimi bado nipo ingawa sijui wao wana mpango gani na mimi nataka kuendelea kuwa hapa,”

Previous articleMWAMBA HUYU KUCHUKUA MIKOBA YA SAKHO SIMBA
Next articleSINGIDA UNITED CHIMBO LAO ARUSHA