Home Sports MATOLA:WACHEZAJI WANAFURAHIA MAZOEZI,KESHO TENA

MATOLA:WACHEZAJI WANAFURAHIA MAZOEZI,KESHO TENA

SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wachezaji wamezidi kuyafurahia mazoezi ambayo wanayafanya nchini Misri na wanapiga hatua kila wakati.

Kikosi hicho kwa sasa kipo nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2022/23 ambao unatarajiwa kuanza Agosti.

Matola amesema:”Kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wanayafurahia mazoezi kwa sasa ambayo tunayafanya na tulianza kidogokidogo sasa tumeanza kufanya mazoezi makubwa.

“Kikubwa ni kuona kila mchezaji anakuwa imara na hilo tunalifanya kwa sasa,tuna amini kwamba kwa mechi za kirafiki ambazo tunacheza tunazidi kuwa imara zaidi,” amesema.

Kesho Julai 27 kikosi cha Simba kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Klabu ya Haras El Hodoud ambao utapigwa jijini Cairo

Previous articleKOCHA MPYA TANZANIA NI MRUNDI
Next articleCRDB WAFURAHIA TUZO,WAIREJESHA KWA WATEJA