BARCELONA wamefikia hatua nzuri ya kuipata saini ya staa wa Bayern Munich, Robert Lewandowski kwa ajili ya kuwa naye kwenye kikosi hicho.
Ni kandarasi ya miaka mitatu wamefikia makubaliano ya kumpa mkataba mshambuliaji huyo.
Wakati wowote kuanzia sasa Klabu ya Barcelona watamtangaza rasmi Lewandowski.
Nyota huyo alikuwa amesaliwa na kandarasi ya mwaka mmoja ndani ya Bayern Munich ambao wameweka wazi kwamba wamefikia makualiano mazuri na Barcelona kwa ajili ya mchezaji huyo kujiunga na timu hiyo.
Staa huyo ni raia wa Poland anatajwa kujiunga na Barcelona kwa euro 45 milioni na itaongezwa nyingine 5 kufanya iwe euro milioni 50 ikumbukwe kuwa alifunga mabao 35 msimu uliopita alipokuwa ni mfungaji bora ndani ya Bundesliga.
Team Canada forward Jonathan David (#7) watches as his shot is saved by the Iceland goalkeeper during an international friendly match between Canada and Iceland at BMO Field in Toronto, Ontario, Canada, on March 28, 2026. (Photo by Indrawan Kumala/NurPhoto) (Photo by Indrawan Kumala / NurPhoto via AFP)