Home Sports BANDA APATA TIMU AFRIKA KUSINI

BANDA APATA TIMU AFRIKA KUSINI

 MTANZANIA Abdi Banda amepata changamoto mpya kwa ajili ya kuonyesha uwezo wake kwa msimu mpya wa 2022/23.

Banda ambaye ni nyota wa zamani wa Baroka FC ya Afrika Kusini amesaini mkataba wa miaka 2 kuichezea timu ya Chippas United inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

 Kabla ya kujiunga na Chippas Banda aliwahi kukipiga pia Highland Park na msimu wa 2021/22 alikuwa ndani ya Klabu ya Mtibwa Sugar ya Tanzania.

Banda amesema:-“Nimesaini miaka miwili. Nafurahi nimerudi, naomba Watanzania wote waniunge mkono na kunipa sapoti sababu sio kazi nyepesi.

“Kikubwa watusapoti na sisi wazawa. Wategemee ujio mwingine na kuona tofauti kubwa,” amesema

Previous articleISHU YA KAMBI YA YANGA MORO IPO HIVI
Next articleMVP BANGALA DAKIKA ZAKE BONGO KWENYE LIGI