Home Uncategorized SADIO MANE APANDIWA DAU TENA NA BAYERN MUNICH

SADIO MANE APANDIWA DAU TENA NA BAYERN MUNICH

BAYERN Munich wanajiandaa kuwasilisha ofa kwa ajili ya kumpata winga Sadio Mane ambaye anakipiga ndani ya Liverpool inayoshiriki Ligi Kuu England.

Ni zaidi ya pauni milioni 30 zimetengwa na Bayern Munich kwa ajili ya kumpata mchezaji huyo raia wa Senegal ambaye anahitaji kuondoka hapo.

Dau la kwanza lilikuwa pauni milioni 30 mabosi wa Liverpool waliligomea hivyo kwa sasa mabosi wa Bayern wanajiandaa kupeleka dau jipya na la maana.

Inatajwa kwamba mezani wanataka kuwekewa pauni milioni milioni 42 mabosi wa Liverpool ili waweze kumuachia nyota huyo.

Mane amebakiza miezi 12 ndani ya Liverpool kukamilisha mkataba wake na amedokeza kuwa anahitaji kuwa mahali pengine.

Previous articleZLATAN BADO YUYUPO AC MILAN
Next articleBANDA AINGIA ANGA ZA YANGA