Home Sports ZLATAN BADO YUYUPO AC MILAN

ZLATAN BADO YUYUPO AC MILAN

NYOTA wa Klabu ya AC Milan,Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kuendelea kutumika ndani ya kikosi hicho kwa msimu mwingine tena kwa mujibu wa taarifa.

Nyota huyo mwenye miaka 40 alifanyiwa upasuaji wa goti Mei 25 mwaka huu na anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita.

Staa huyo msimu wa 2021/22 licha ya majeraha ya mara kwa mara alikuwa chachu ya mafanikio ya timu hiyo kuweza kutwaa ubingwa wa Serie A.

Inaelezwa kuwa Zlatan amekubali kukatwa mshahara na kupunguziwa bonasi ili aweze kuongeza mkataba ndani ya timu hiyo.

Previous articleNAMNA CAF WALIVYOWEKA ZUIO KOCHA MPYA SIMBA
Next articleSADIO MANE APANDIWA DAU TENA NA BAYERN MUNICH