PABLO:TUNAZITAKA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Ni mchezo wa mzunguko wa pili kwa Pablo mbele ya Kagera Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Francis Baraza.

Akizungumza na Saleh Jembe, Pablo amesema kuwa wanatambua kwamba ligi ni ngumu na kila timu inahitaji kupata ushindi hivyo watafanya vizuri mchezo huo.

“Tunahitaji kupata pointi tatu na tunajua kwamba utakuwa mchezo mgumu kikubwa ambacho tutakifanya ni kubadili mbinu na kucheza mchezo mzuri.

“Wachezaji wapo tayari na wamekuwa wakifanya mazoezi kwa ajili ya mechi ambayo nafuata hasa ukizingatia kwamba mchezo wetu mbele ya Ruvu Shooting tulipata ushindi.

“Ushindi wa mabao 4-1 kwetu ni mkubwa na mzuri hivyo ambacho tunapaswa kukifanya ni kuendelea pale ambapo tuliishia kwenye mchezo wetu,” amesema.

Kwenye mchezo huo bao la ufunguzi lilifungwa na Kiu Dennis na lile la Ruvu Shooting lilifungwa na Haruna Chanongo.