Home International KLOPP ANAAMINI WAPINZANI WATASHANGILIA SARE UEFA CHAMPIONS LEAGUE

KLOPP ANAAMINI WAPINZANI WATASHANGILIA SARE UEFA CHAMPIONS LEAGUE

JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa anajua kwamba wapinzani wake watakuwa wanasherehekea sare waliyopata katika mchezo wa UEFA Champions League.

Ilikuwa ni hatua ya robo fainali ya pili na ubao wa Uwanja wa Anfield ulisoma Liverpool 3-3 Benfica na sare hiyo iliwapa nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali kwa jumla ya mabao 6-4.

Watupiaji walikuwa ni Ibrahima Konate dk 21,Robert Firmino alitupia mawili ilikuwa dk ya 55 na 65.

Benfica hawakuwa wanyonge walitupia mabao kupitia kwa Goncalo Ramos dk 32,Roman Yaremchuk dk 73 na Darwin Nunez dk 81.

Klopp amesema:”Labda ilikuwa vile ambavyo tulikuwa tunataka kufanya lakini haikuwa jambo la muhimu sana. Kucheza mchezo mzuri au kucheza kwa umakini muda wote lakini ambacho tunakitaka ni kwenda fainali.

“Ni ngumu kuwa katika ubora asilimia 100 ila ninajua kwamba wapinzani wetu watashangilia kwa kuwa wamepata sare haya ni matokeo lakini hatukuwa katika ubora wetu,”.

Liverpool itakutana na Villarreal katika mchezo wa nusu fainali. Villarreal inayonolewa na Kocha Mkuu, Unai Emery iliwafungashia virago Bayern Munich kwa jumla ya mabao 2-1.

Previous articleYANGA:TUNAZITAKA POINTI TATU ZA SIMBA
Next articleCITY YATINGA NUSU FAINALI UEFA CHAMPIONS LEAGUE