Home International CITY YATINGA NUSU FAINALI UEFA CHAMPIONS LEAGUE

CITY YATINGA NUSU FAINALI UEFA CHAMPIONS LEAGUE

MANCHESTER City inayonolewa na Kocha Mkuu,Pep Guardiola inatinga hatua ya nusu fainali baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Atletico Madrid.

City inakata tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya UEFA Champions League ikiwa katika Uwanja wa Wanda Metropolitan kwa jumla ya bao 1-0 .

Manchester City beki wao John Stones amesema kuwa licha ya kupata sare waliweza kustahimili presha.

“Ninajivunia katika hili hasa kwa namna ambavyo tumeweza kuhimili presha ya mchezo uliokuwa mgumu. Ni furaha kuweza kufanya jambo kubwa,”.

Guardiola amesema kuwa mtindo ambao wanacheza Atletico Madrid ni mgumu na wanacheza vile ambavyo wanataka.

Kocha Mkuu wa Atletico Madrid, Diego Simeone amesema hana sababu ya kutoa maoni kuhusu kuwa ni jambo zuri ama jambo baya.

“Lakini hawa ambao wanaona namna hali ilivyokuwa wanasema mengi inaweza kuwa wanaona labda sisi tupo tofauti,”.

Previous articleKLOPP ANAAMINI WAPINZANI WATASHANGILIA SARE UEFA CHAMPIONS LEAGUE
Next articleAIR MANULA KATIKA ANGA ZA KIMATAIA KAKIWASHA