AIR MANULA KATIKA ANGA ZA KIMATAIA KAKIWASHA

    HAKUNA anayejua itakuaje sasa kwenye hatua ya robo fainali baada ya Simba kufanikiwa kupenya hasa kwenye upande wa lango nani ataanza kati ya Aishi Manula,Beno Kakolanya ama Ally Salim.

    Weka kando kuhusu kufikiria nani ataanza lakini chaguo namba moja ni Manula ambaye amekuwa kwenye mwendelezo bora awapo langoni.

    Hapa tunakuletea namna nyota huyo alivyotimiza majukumu yake katika anga la kimataifa:-

    Dk 900 zimeyeyuka

    Mechi 10 dk 900 akiwa ameweza kuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Simba,Pablo Franc ambaye ameweza kuandika rekodi ya kuipelekea timu hiyo hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho.

    Manula kwenye mechi za kimataifa ambazo amekaa langoni ametunguliwa mabao ya kufungwa 12 akiwa na wastani wa kuokota langoni bao moja kila baada ya dakika ya 75.

    Aliweza kushuhudia timu hiyo ikiweza kufunga jumla ya mabao 16 ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dk 56 ni kwenye mechi zote kuanzia ligi ya mabingwa mpaka Kombe la Shirikisho.

    Katika mechi hizo ambazo alikaa langoni ni mechi 4 aliweza kukamilisha dk 90 bila kufungwa na alifungwa kwenye mechi 6.

    Mwendo wake ulikuwa hivi:-

    Ligi ya Mabingwa

    Dakika 180 kwenye Ligi ya Mabingwa Manula aliweza kuanza langoni na mchezo wa kwanza ugenini aliweza kukamilisha bila kufungwa ila ule wa pili Uwanja wa Mkapa hakuwa na chaguo.

    Mchezo wa kwanza ubao Oktoba 17 ulisoma Jwaneg Galaxy 0-2 Simba ilikuwa ugenini na ule wa pili Simba 1-3 Jwaneng Galaxy ilikuwa ni Oktoba 24,2021, hapa Manula alishuhudia timu hiyo ikifungashiwa virago Ligi ya Mabingwa Afrika.

    Hatua ya mtoano

    Novemba 28,2021 ubao ulisoma Simba 3-0 Red Arrows na kete ya pili Red Arrows 2-1 Simba alikamilisha dk 180 kwa mara nyingine tena na timu hiyo iliweza kutinga hatua ya makundi.

    Hatua ya makundi

    Mechi zote sita dk 540 alianza langoni ilikuwa ni Februari 13,2022 ngoma ilikuwa Simba 3-1 ASEC Mimosas kigongo cha Februari 20,2022 Simba 1-1 USGN.

    Februari 27,2022, RS Berkane 2-0 Simba mchezo wa Machi 13,2022 ilikuwa Simba 1-0 RS Berkane kkete nyingine ya Machi 20,2022,ASEC Mimosas 3-0 Simba.

    Kwenye mchezo huu Manula aliweza kuwa shujaa kwa kuwa aliokoa penalti mbiliya kwanza ni yeye mwenyewe aliisababisha na alionyeshwa kadi ya njano moja ilikuwa dk ya 35 ile ya pili ilisababishwa na Joash Onyango.

    Alifunga ukurasa wa kukamilisha mechi 10 za kimataofa Aprili 3,2022 na Uwanja wa Mkapa ilikuwa Simba 4-0 USGN.

    Kwenye mchezo huu Manula aliweza kuwa imara langoni ambapo aliweza kuokoa michomo ya mshambuliaji tegemeo wa USGN, Victorean Adebayo ilikuwa n idk ya 44.

    Kituo kinachofuata

    Manula ana kazi nyingine mbele ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini ikiwa ni hatua ya robo fainali na kwenye hatua hii Simba itaanza kutupa karata yake ya kwanza ikiwa Uwanja wa Mkapa na ile kete ya mwisho itachezwa Afrika Kusini.

    Mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa Aprili 17,2022 kisha ule wa pili itakuwa ni Aprili 27,2022.

    Manula amesema kuwa ushirikiano anaoupata kutoka kwa wachezaji pamoja na uwepo wa mashabiki vinawapa nguvu ya kufanya vizuri.

    “Ninaweza kusema kwamba malengo yetu ni kuona tunafika mbali kwenye haya mashindano ya kimataifa lakini haitoke hivihivi bali ni ule ushirikiano kutoka kwa wachezaji,benchi la ufundi pamoja na mashabiki ambao wapo pamoja nasi,”.

    Previous articleCITY YATINGA NUSU FAINALI UEFA CHAMPIONS LEAGUE
    Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA