MILANGO YA USHIRIKA MIGUMU MWANZO MWISHO, POLISI TANZANIA 0-0SIMBA

UWANJA wa Ushirika Moshi,milango kwa timu zote mbili ilikuwa migumu mwanzo mpaka mwisho wa mchezo na kufanya timu zote zigawane pointi mojamoja.

Ubao umesoma Polisi Tanzania 0-0 Simba ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa 19 msimu wa 2021/22.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara sasa wanafikisha pointi 41 wakiwa wameachwa kwa jumla ya pointi 10.

Yanga ni namba moja wana pointi 51 na wote wamecheza mechi 19 ndani ya msimu huu ambao kazikazi inaendelea.