Home International KIMATAIFA SIMBA YAPIGA MASHUTI 20

KIMATAIFA SIMBA YAPIGA MASHUTI 20

NYOTA wa Simba wanaonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi mbele ya USGN rekodi zinaonyesha kwamba walipiga mashuti 20 langoni kwa wapinzani wao.

Haikuwa kazi rahisi kwa Simba kuweza kufanikisha lengo lao kwa kuwa kipindi cha kwanza safu ya ushambuliaji ilikosa umakini ndani ya dakika 45 licha ya kupata nafasi kwenye mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki waliojitokeza usiku.

Katika mashuti 20 ambayo Sima walipiga ni 6 pekee yaliweza kulenga lango ambapo kwa kipindi cha kwanza ni shuti moja tu lililenga lango na ni mabao 4 walifunga huku wachezaji wa Sima wao wakitupia mabao 3.

Bao moja ni mali ya nyota wa USGN Saidu Hamisu ambaye alijifunga katika harakati za kuokoa mpira ambao alirudishiwa na beki wake mwenyewe.

Mabao ya Simba yalifungwa na Sadio Kanoute pamoja na Chris Mugalu ambaye aliweza kufunga mabao mawili kwenye mchezo huo.

Mzee wa kukera Bernard Morrison aliweza kutoa pasi mbili za mabao katika mchezo huo moja alimpa Kanoute na moja alimpa Mugalu.

Previous articleTOTTENHAM YASHINDA 5G,YATINGA 4 BORA
Next articleZIMETINGA ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO,KUKUTANA NA SIMBA