TOTTENHAM YASHINDA 5G,YATINGA 4 BORA

TOTTENHAM Hotspur imeishushia kichapo cha mabao 5-1 Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Mchezo huo umechezwa usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa Tottenham Hotspur mbele ya mashabiki 57,553.

Mabao ya Ben Davies dk 43,Matt Doherty dk 48,Heung-min Son dk 54,Emerson Leite de Souza Junior dk 63,Steven Bergwijn dk 83 ambaye alianzia benchi yalitosha kuipa ushindi Spurs.

Waliotangulia kufunga katika mchezo walikauwa ni Newcastle United dk ya 39 na Fabian Schar alipiga pigo huru lililozama nyavuni na likawa bao pekee kwao.

Tottenham inakuwa nafasi ya nne na pointi 54 huku Newcastle United ikiwa nafasi ya 15 na pointi 31 zote zimecheza mechi 30.