MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa yeye sio mcheza kamali hivyo hawezi kutabiri jambo lolote kuhusu matokeo.
Kocha huyo kesho Machi 16 ana kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu England.
Arteta amesema:”Naona kwa sasa unaona kwamba tumekuwa na muda wa kuwa pamoja na tunafurahia kucheza lakini suala la kubashiri hilo kwangu halipo.
Arsenal imekuwa katika ubora hivi karibuni ambapo Machi 13 iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Leicester City na watupiaji walikuwa ninThomas Partey dk 11 na Alexandre Lacazette dk 59 kwa penalti.
“Mchezo wetu ujao, (Liverpool) utakuwa ni mgumu na nikitazama ratiba naona namna ambavyo tumebakiwa na mechi kadhaa lakini hilo halitupi mashaka.
“Kikubwa ambacho tunaangalia ni kwa ajili ya mechi za mbele na tunahitaji kucheza katika kiwango bora,mimi sio mcheza kamali na wala sifikirii kucheza kamali,”.
Related News
Tottenham Hotspur forward Dominic Solanke battles with Crystal Palace defender Maxence Lacroix during the English championship Premier League football match between Crystal Palace and Tottenham Hotspur on 27 October 2024 at Selhurst Park in London, England - Photo Ian Stephen / ProSportsImages / DPPI (Photo by IAN STEPHEN / ProSportsImages / DPPI via AFP)