Feisal Salum ni King of Asisti NBC Premier League

Rekodi zinazidi kuandikwa ndani ya Tanzania Premier League ambayo ni ligi namba 6 kwa ubora Afrika.

Wakati timu mbili zikiwa hazijapoteza ndani ya ligi, Yanga SC na Azam FC kinara kwenye kutengeneza pasi za mwisho maskani yake ipo Azam Complex kwenye mechi za nyumbani.

Ni Kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum huyu ni King of Asisti NBC Premier League akiwa amefikisha jumla ya pasi 7.

Mbali na kutengeneza pasi kwa wengine amefunga magoli 7. Jumla amehusika katika magoli 14 kati ya 26 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya 3 kwenye msimamo.

Kwa sasa ligi imesimama kwa muda kutokana na Muungano Cup 2026 burudani inatarajiwa kurejea hivi punde mara baada ya mashindano hayo kufika ukingoni.

Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi ni Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Pedro Goncalves na Azam FC ni miongoni mwa timu ambazo zitaanzia hatua ya robo fainali.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.