Home Uncategorized NG’OMBE WA MAYELE ATUA DAR LEO

NG’OMBE WA MAYELE ATUA DAR LEO

SHABIKI wa Yanga  kutoka Morogoro aliyeahidi kumzawadia mchezaji Fiston Mayele Ng’ombe mmoja baada ya kufunga bao katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, ametimiza ahadi na kumfikisha Ng’ombe huyo leo Machi 14, 2022.

Ni katika makao makuu ya Klabu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es Salaam zawadi imefika kwa ajili ya kutimiza ahadi ya muda kidogo.

Mayele alipewa ahadi ya kupewa Ng’ombe na shabiki huyo, baada ya kufunga bao katika mechi iliyochezwa Februari 23, mwaka huu katika Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Pia shabiki huyo amekabidhi mbuzi mmoja kwa ajili ya Rais na Mkurugenzi wa GSM, Ghalib Said Mohamed, ikiwa ni pole kwa kufiwa na baba yake mzazi, Said Mohamed.

Mayele amesema kuwa zawadi hiyo ni pongezi kubwa na inaongeza morali kwake pamoja na wachezaji kiujumla.

“Ni furaha kwetu kuona zawadi nimepata na ni kwa ajili ya kuongeza morali hivyo tutazidi kupambana zaidi kupata matokeo,” amesema Mayele.

Previous articleVIDEO:SIMBA ULAYA NA NENO LAKE HILI,PASI MILIONI
Next articleYANGA WAJA NA MFUMO MPYA WA UCHAGUZI