Home Sports YANGA WAJA NA MFUMO MPYA WA UCHAGUZI

YANGA WAJA NA MFUMO MPYA WA UCHAGUZI

KLABU ya Yanga kwa sasa ipo kwenye mchakato wa uchaguzi ambapo imeweka wazi kuwa kutakuwa na mfumo mpya utakaotumika katika upigaji kura.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Malangwe Mchungahela amesema kuwa yote hayo ni kutokana na mabadiliko ya katiba ambayo imepitishwa na wanachama.

“Uchaguzi wa matawi unatakiwa kuanza Machi 18 2022 hadi mwishoni mwa mwezi wa 4 hapo wanatakiwa wawe wameshamaliza kufanya uchaguzi na vigezo ni kujua kusoma na kuandika,kuwa mwanachama hai,kutokuwa na makosa ya jinai na nyingine zipo kwenye katiba.

“Tumebadilisha mfumo wetu wa upigaji kura na sasa uchaguzi utaanzia kwenye matawi kwa nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu,Katibu Msaidizi,Muweka Hazina na Wajumbe Wanne.

“Upigaji kura kwa Rais na Makamu ni wale ambao watachaguliwa kutoka kwenye matawi ambao ni viongozi, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mweka Hazina na Katibu pamoja na Wajumbe wawili mmoja lazima awe Mwanamke,” amesema.

Previous articleNG’OMBE WA MAYELE ATUA DAR LEO
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE, MACHI 15,2022