LICHA ya kuwa nyuma jana mbele ya Morocco kwa bao lililofungwa dakika ya 6 na Soufiane Boufal Misri iliweza kupindua meza na kuibuka na ushindi.
Baada ya dakika 90 kukamilika Misri iliweza kushinda mabao 2-1 na kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe Afcon 2021.
Ni Mohamed Salah aliweza kusawazisha dakika ya 56 kisha mchezo ukafika katika dakika za nyongeza ndipo Mahmoud Trezeguet alifunga dakika ya 100.
Bao hilo lilifanya mchezo huo kutofika katika hatua ya matuta na hivyo Misri inatinga hatua ya nusu fainali na watakutana na wenyeji Cameroon mchezo utakaochezwa Februari 3.