Home Sports POLISI TANZANIA V YANGA KUPIGWA SHEIKH AMRI ABEID

POLISI TANZANIA V YANGA KUPIGWA SHEIKH AMRI ABEID

MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Polisi Tanzania dhidi ya Yanga unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Awali mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ushirika, Moshi kutokana na uwanja huo kuwa na matumizi mengine sasa mchezo utachezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kwa namna kikosi chao kilivyojipanga hawana mashaka na sehemu ambayo watapangiwa kuchezwa wao wanataka pointi tatu.

“Sisi hatuna tatizo na sehemu ambayo tutapangiwa kucheza ambacho tunakitaka sisi ni pointi tatu hata wakitupeleka Bunju hatuna tatizo.

“Kazi yetu sisi sio kupanga ama kuchagua uwanja kazi yetu sisi ni kucheza mpira na kuchukua pointi tatu hakuna jambo lingine,”.

Msimu uliopita mchezo wao walipokuwa ugenini ulichezwa Uwanja wa Ushirika Moshi na ubao ulisoma Polisi Tanzania 0-0 Yanga.

Previous articleLIGI KUU TANZANIA BARA LEO RATIBA
Next articleBEKI WA KAZI KIMENYA KUIKOSA AZAM FC