>

LIGI KUU TANZANIA BARA LEO RATIBA

JANUARI 22, Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea na kutakuwa na kazi kubwa katika viwanja vitatu tofauti kwa timu kusaka pointi tatu.

Ni Mtibwa Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Salum Mayanga itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Pablo Franco.

Ngoma ya Mtibwa Sugar v Simba itapigwa Uwanja wa Manungu.

Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 13 na pointi 11 itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Azam FC iliyo nafasi ya 5 ba pointi 18 Uwanja wa Nelson Mandela.

Biashara United itakuwa na mchezo dhidi ya Geita Gold na utapigwa Uwanja wa Karume,Mara.

Biashara United ipo nafasi ya 15 na pointi 10 inakutana na Geita Gold iliyo nafasi ya 10 na pointi 13.