>

DAKIKA 45:MTIBWA SUGAR 0-0 SIMBA

UWANJA wa Manungu dakika 45 zimekamilika kwa timu zote kuenda mapumziko wakiwa wametoshana nguvu.

Ubao unasoma Mtibwa Sugar 0-0 Simba mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Timu zote zipo kwenye ubora ambapo Uwanja wa Manungu ni changamoto kwa timu zote mbili.

Kiungo Said Ndemla wa Mtibwa Sugar ni moto mkali ndani ya dakika 45 huku Inonga Banka akiwa katika kazi kubwa kuzuia.

Shaban Kado langoni amekuwa imara kama ilivyo Aishi Manula wa Simba.