>

MANUNGU MILANGO MIGUMU,MTIBWA SUGAR O-0 SIMBA

UWANJA wa Manungu milango ni migumu kwa timu zote mbili hakuna ambaye ameona lango.

Wanagawana pointi mojamoja katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliokuwa na ushindani mkubwa.

Aishi Manula na Shaban Kado hawa wote wameibuka na ushujaa kwa kuwa hakuna ambaye ameokota mpira wavuni.

Simba ina kibarua kizito sasa kwa Kagera Sugar mchezo unaofuatwa  na hali inazidi kuwa tete kwani licha ya uwepo wa Chama Clatous ngoma ilikuwa ngumu Matokeo haya yanaifanya Simba wafikishe pointi 25 nafasi ya pili Mtibwa Sugar pointi 12 nafasi ya 13.

Yanga ni vinara wakiwa na pointi 32 baada ya kucheza mechi 12 na kesho wana kibarua mbele ya Polisi Tanzania..