LIGI Kuu Tanzania Bara bado inaendelea na leo Januari 20 kutakuwa na mchezo mmoja kwa timu kusaka pointi tatu muhimu.
Mbeya City ambayo imetoka kutibua rekodi za Simba kwa kuwatungua kwenye mchezo uliopita Januari 17 kwa bao 1-0 leo itamenyana na Ruvu Shooting.
Mbeya City iliweza kusepa na pointi tatu mazima kwa ushindi huo na bao pekee lilifungwa na Paul Nonga ilikuwa dakika ya 19.
Inakutana na Ruvu Shooting wazee wa mpapaso wakiwa wametoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wao wa ligi uliopita, Uwanja wa Mabatini.
Kwenye msimamo wa ligi Mbeya City imejijimbia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 19 inakutana na Ruvu Shooting iliyo nafasi ya 14 na pointi 11.