>

MCHEZO WA KIRAFIKI, YANGA 0-0 MBUNI FC

MCHEZO wa kirafiki kati ya Yanga v Mbuni kwa sasa ni mapumziko Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Mchezaji wa Mbuni Hussein Idd ameonyeshwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza baada ya kumchezea faulo mchezaji wa Yanga David Bryson.

Kiungo mshambuliaji Dickosn Ambundo alifanya jaribio la kwanza na matata kwa upande wa Yanga lakini liliokolewa na kipa wa Mbuni FC.

Kiungo Chico Ushindi ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo benchi leo huku Sure Boy akianza kikosi cha kwanza.

Kwenye benchi la ufundi ni Kocha Nasreddine Nabi ambaye anakwenda kuwapa mbinu wachezaji wake ili kuweza kuona watapata jambo gani.