>

FT:MBUNI FC 0-2,MUKOKO ATUPIA MBILI

UWANJA wa Sheikh Amri Abeid dakika 90 zimekamilika kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Mbuni ambapo ni Yanga wameibuka kidedea kwenye mchezo wa leo.

Mabao yote ya Yanga yamefungwa kipindi cha pili kwa kuwa dakika 45 za mwanzo timu zote zilitoshana nguvu na mtupiaji ni Mukoko Tonombe ambaye alifunga mabao hayo kwa penalti dakika ya 56 na 82.

Mbuni walikamilisha dakika 90 wakiwa pungufu baada ya mchezaji wao mmoja kuonyeshwa kadi nyekudu ya moja kwa moja baada ya kumchezea faulo mchezaji wa Yanga.

David Bryson alikutana na mguu wa shingo mguu wa roho dakika ya 36 kutoka kwa nyota wa Mbuni FC Hussein Idd.

Mashuti manne kwa Mbuni yalilenga lango na 7 yalilenga lango kwa upande huku manne yakitoka nje ya lango kwa upande wa Mbuni na mawili kwa upande wa Yanga.

Mchezo huo ulikuwa mubashara kupitia Azam TV moja kwa moja kutoka Arusha.