Home Sports KOCHA AZAM FC AIBUKIA BIASHARA UNITED

KOCHA AZAM FC AIBUKIA BIASHARA UNITED

BIASHARA United imemtambulisha rasmi Vivier Bahati kuwa kocha mkuu wa timu hiyo na tayari ameanza kazi rasmi kuinoa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara.

Bahati alikuwa anainoa timu ya Azam FC mkataba wake ulivunjwa kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo na waliondoka pamoja na Kocha Mkuu, George Lwandamina.

Anachukua mikoba ya Patrick Odhiambo ambaye amebwaga manyanga hivi karibuni ndani ya timu hiyo inayotumia Uwanja wa Karume,Mara.

Vivier Bahati amepewa dili la miezi sita kwa ajili ya kuinoa timu hiyo iliyo nafasi ya 15 na pointi 10.

Mchezo wake ujao ni dhidi ya Geita Gold na utachezwa Uwanja wa Karume itakuwa ni Januari 22.

Previous articleFT:MBUNI FC 0-2,MUKOKO ATUPIA MBILI
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMIS