YANGA:TUNA KIKOSI IMARA CHA KAZI,YAFUNGUKIA ISHU YA CHAMA

THABIT Kandoro, Mkurugenzi wa Mashindano ndani ya kikosi cha Yanga ameweka wana kikosi imara cha kazi ambacho kitawapa mafanikio kwa muda mrefu.

Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza mechi 12 imetoka kushinda mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kandoro amesema kuwa kikosi chao ni imara na kina wachezaji wazuri.

“Kikosi ni imara na kina wachezaji wazuri ambao wanapambana kusaka matokeo kwa hapa tulipo ninaweza kusema kwamba bado tuna kazi ya kuendelea kufanya na tuna amini kila kitu kitakuwa sawa,”.

Hivi karibuni Yanga ilikuwa inatajwa kuwania saini ya Chama Clatous kiungo aliyekuwa anakipiga ndani ya RS Berkane lakini ametambulishwa ndani ya Simba.

Kuhusu hilo aliweka wazi kwamba hawakuwa na hesabu za kumsajili mchezaji huyo.