Home Sports SALAH AVUNJA UKIMIYA LIVERPOOL

SALAH AVUNJA UKIMIYA LIVERPOOL

MOHAMED Salah amesema hatma yake ndani ya Liverpool iko mikononi mwaka bodi ya klabu hiyo, ila yeye anapenda kuendelea kubaki Anfield.

Ishu ya Salah kusaini mkataba mpya ndani ya Liverpool imekuwa ikizungumzwa tangu mwaka jana lakini hakuna muafaka uliofikiwa mpaka sasa.


Salah
anatarajiwa kumaliza mkataba wake ndani ya miezi 18 ijayo katika klabu hiyo na yeye anatamani kustaafia soka lake hapo.


Staa huyo alitua
Liverpool mwaka 2017 akitokea Roma kwa pauni 34m.


Inaelezwa kuwa katika
mkataba wake mpya nyota huyo anadaiwa kuhitaji kiasi cha mshahara wa pauni 350,000 kwa wiki na
atakuwa mchezaji ambaye
analipwa vizuri kwa muda wote ndani ya
Liverpool.
Salah amesema: “Nataka kubaki hapa, ila maamuzi
hayapo mikononi
mwangu. Wanafahamu ninachotaka sijaomba
vitu vya kutisha
nimeomba kile kitu ambacho wana uwezo
nacho na sio vinginevyo.


“Nimekuwa hapa
kwa msimu wa tano sasa, naifahamu klabu
yangu vizuri, nawapenda
mashabiki, lakini uongozi
wao unajua hali halisi
na wao ndiyo watafanya maamuzi.”

Previous articleDTB YAPANIA KUZIPIKU SIMBA, YANGA
Next articleKITAWAKA MAPINDUZI CUP LEO, SIMBA NA AZAM