KITAWAKA MAPINDUZI CUP LEO, SIMBA NA AZAM

MADOA MADOA yote yaliyojificha yatajulikana leo kutokana na balaa ambalo linakwenda kufanywa na nyota hawa ambao wanapewa nafasi ya kukinukisha katika fainali ya Kombe la Mapinduzi.


Hapa Spoti Xtra linakuletea nyota wa
Simba na Azam FC ambao wanatarajiwa kusaka mbabe atakayesepa na taji hilo
katika fainali itakayochezwa kwenye
Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

SIMBA SC
Aishi Manula
Ni kipa namba moja wa Simba, anapewa nafasi ya kuanza langoni leo kutokana na mwendo wake kuwa bora
ndani ya Kombe la Mapinduzi.


Simba ikiwa imecheza mechi tatu,
yeye ameanza langoni kwenye mechi mbili ambazo ni sawa na dakika 180 akicheza dhidi ya Mlandege na Namungo FC, mechi zote hizo hakuruhusu bao.
Anakumbukwa namna alivyoonesha
balaa katika kuokoa hatari mbele ya Namungo FC ilikuwa ni dakika ya 42,
56, 60, 74 na 88 na kulifanya lango lake
kuwa salama.

 

Rally Bwalya Anautumia vema mguu wake wa kushoto. Amecheza mechi mbili dhidi ya Selem View na Namungo. Amefunga
bao moja kwa mguu wa kushoto akiwa
nje ya 18, ilikuwa dhidi ya Selem View.

Meddie Kagere Mzee wa kukaa kwenye nafasi hasa pale anapokuwa na viungo wa kumtengeneza mabao, alifunga
bao mbele ya Namungo
FC na kuongeza nguvu kwa
Simba
kutinga fainali.

Pape Sakho Nyota ambaye amekuwa na hatari kila awapo uwanjani, amefunga mabao mawili kwenye michuano hii akiwa ni
kinara wa utupiaji kwa
upande wa Simba.


Mbele ya Selem
View na Namungo alifunga, hivyo ana balaa kwenye kila mechi ambazo ameanza. Henock Inonga Beki wa kazi chafu, hana maswali mara mbilimbili kwenye kuanua hatari zinapofika miguuni mwake, ana spidi katika kupanda na kushuka.
Jonas Mkude
Mmiliki wa eneo la kati, kazi chafu zinatengenezwa kwake. Kakinukisha kwenye mechi zote tatu akianza kikosi cha kwanza na hajashuhudia timu yake ikifungwa.


Sadio Kanoute
Kukiwa na migongano mingi huwezi kumuona Kanoute labda ataibukia kwenye kona kwa kuwa ni mtu wa kugusa na kuachia.


Kibu Dennis
Ni chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Pablo Franco
na amekuwa akiwapa tabu
mabeki wa timu pinzani pale
wanapokutana.

 

AZAM FC Frank Domayo Moja ya nyota wa kazi chafu
ndani ya Azam FC. Alionyesha
balaa kwenye mchezo wa nusu
fainali wa Kombe la Mapinduzi
mbele ya Zawad Mauya ambapo
alimchezea faulo mbaya dakika
ya 69. Ni mpambanaji.
Daniel Amoah

Hana mambo mengi, yeye anapiga kazi tu, anapanda na kushuka, kibindoni ana bao moja.

Tepsi Evance Lile balaa aliloonesha mbele ya Yanga kwenye
hatua ya nusu
fainali kwa mabeki halikuwa la kitoto. Anautumia vema mguu wake wa kushoto.


Ibrahim Ajibu
Jamaa huyu ni mzee wa kujibu majibu ya wana Azam FC kwa sasa akiwa anapewa nafasi ya kuanza mbele ya mabosi wake wa zamani.

Alipokutana na mabosi wake wa zamani Yanga kwenye
mchezo wa nusu fainali ya Kombe
la Mapinduzi alipewa jukumu la
kupiga faulo, yeye alicheza faulo
tatu na kuoneshwa kadi ya njano
dakika ya 67.


Edward Manyama
Kinara wa pasi za mwisho ndani ya Azam FC kwenye Kombe la Mapinduzi akiwa nazo mbili kati ya mabao 7. Kazi ya mipira iliyokufa itakuwa kwenye miguu yake katika
kuonesha balaa.

Idris Mbombo Ingizo jipya ndani ya Azam FC linakwenda kupambana na mshikaji wake Inonga ambaye naye ni raia wa
DR Congo, ametupia
mabao mawili.


Agrey Morris
Kisiki wa kazi ukuta wake mpaka sasa umeruhusu kufungwa bao moja kwenye mechi nne ambazo Azam FC imecheza.


Mathias Kigonya
Hakuwa na bahati ya kuokoa penalti mbele ya
Yanga kwa kuwa Yassin
Mustapha alipaisha lakini umbo lake la miramba minne likiwa langoni linatisha