KUFUATIA mwenendo mzuri wa usajili waunaofanywa
DTB, mwenyekiti wa klabu hiyo, Ibrahim Mirambo amejigamba
kuwa, wamepania zaidi kuhakikisha wanamsajili
mchezaji yeyote hata awe chaguo la Simba au Yanga.
DTB ndiyo vinara wa Championship ambapo hadi sasa wanaongoza msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 36,
walizozivuna kwenye michezo 14.
Akizungumza na Spoti Xtra, Mirambo ameweka wazi kuwa:
“Bado tunafanya usajili, sisi kama timu bado hatujatambulisha rasmi nyota yoyote ingawa kweli kuna baadhi wanaonekana tayari wameshajiunga na sisi, kubwa tunahitaji kuwa na kikosi bora ili
tuweze kupanda Ligi Kuu Bara.
“Nia yetu baada ya kupanda tunatarajia kushindana na kufuta dhana ya timu fulani kuwa ndiyo zenye uwezo pekee wa
kusajili na kuchukua makombe makubwa, hivyo nadhani muda
wa utambulisho wa nyota wetu tuliowasajili ukifika kila mmoja
atajua hizo tetesi zinazosemwa.”