SALUM MAYANGA KOCHA MPYA MTIBWA SUGAR

RASMI Salum Mayanga atakuwa kwenye benchi la ufundi la Mtibwa Sugar baada ya kutambulishwa leo Januari 7,2022.

Mayanga alikuwa akiinoa timu ya Tanzania Prisons ambapo alikuwa kwenye mwendo mzuri jambo lililowafanya Mtibwa Sugar kuhitaji huduma yake.

Anachukua mikoba ya Joseph Omong ambaye alichimbishwa Desemba 14,2021.

Kwenye msimamo Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 10 baada ya kucheza mechi 11.